Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na wenzanke wameripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam leo ikiwa ni sehemu ya masharti ya dhamana waliopewa mahakamani katika kesi yao inayowakabili.
Mbowe na viongozi wenzake walifika polisi kwa nyakati tofauti leo asubuhi na kuonekana wakiingia katika ofisi hizo kwa muda kadhaa kisha baadaye wakatoka.
Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzibar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, John heche na Halima Mdee wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe.
Ndani ya makosa hayo, wanadaiwa kufanya mkusanyiko usio halali na uliopelekea maandamano na vurugu zilizosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini na askari polisi kujeruhiwa, Feb. 26.
Akizungumza baada ya kutoka kituoni hapo, Mashinji alismea;
“Mhe. Ester Bbulaya ataunganishwa kwenye shauri hili lakini kwa sasa amebaki kituoni kwa taratibu za kiupelelezi lakini tunafuatilia kwa ukaribu.”
Comments are closed.