The House of Favourite Newspapers

Mbowe: Nimepata Chanjo ya Corona ‘AstraZeneca’

0

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema amepata chanjo ya #COVID19 ya Astrazeneca alipokuwa nje ya nchi kibiashara.

 

 

Akizungumza na vyombo vya habari jana Jumapili, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan aharakishe mchakato wa Uchunguzi dhidi ya Corona ili hatua stahii zichukuliwe mapema na kuepusha vifo vinavyoweza kutokea.

 

 

Amesema awali wao walitaka nchi ichukue hatua stahiki sio kwa maana ya kuifungia nchi bali kuwa na vituo vya kupima watu, kuwa na ventilators za kutosha na vifaa kwa wahudumu wa afya ili kukabiliana na ugonjwa.

 

Leave A Reply