The House of Favourite Newspapers

Mbowe: Rais Samia Alikua Mvumiluvu, Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!-Video

0

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anatambua kuwa ni vigumu kuwaeleza Watanzania na dunia kwamba anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali maridhiano ya kitaifa ila anajivika mabomu kufanya hivyo kutokana na hatua njema iliyofikiwa.

Amesema angeweza kuendeleza msimamo wa mtangulizi wake lakini kutokana na ushawishi wake na wanachadema na viongozi wa CCM wenye busara wamefikia pazuri.

Mbowe ametoa kauli hiyo tarehe 21 Januari, 2023 wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza katika uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara.

Amesema hakuna nchi duniani ambayo imeshawahi kujengwa kwa demokrasia dhoofu kwani demokrasia ikikua na uchumi utakua.

Aidha, amemuomba Rais Samia asikwazike pale ambapo Chadema watampinga kwa nguvu zote katika baadhi ya ajenda.

“Nchi yetu inahitaji Katiba bora, usidanganywe na yeyote kuondoka bila katiba bora, lazima kuwepo na katiba bora ili tusirudi tena kwenye zile chaguzi za kihuni… za watu wanaiba uchaguzi na kuwa huru mitaani.

“Yeyote anayeiba lazima awajibishwe, pale ambapo tunaamini sheria zitasimama kwenye haki wanaostahili, hazitamkandamiza yeyote ili kwa pamoja tulijenge Taifa salama, linaloitengeneza kesho ya watoto wetu kuwa kesho bora zaidi.

“Tutaendelea kuzungumza na ushirikiano lakini tukiwa makini kuliko makini yenyewe.Tutapiga jaramba mpaka kieleweke!” amesema Mbowe.

Leave A Reply