The House of Favourite Newspapers

Mbrazil wa Simba Nje Wiki Tatu

0

KIUNGO mkabaji ndani ya klabu ya Simba, Gerson Fraga, ambaye ni raia wa Brazil, atakuwa nje ya Uwanja kwa muda wa wiki tatu kutokana na majeraha ya goti la mguu wa kushoto aliyopata wakati timu hiyo ilipocheza na Biashara United.

 

Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara,  amesema  Fraga hatafanyiwa upasuaji bali atatibiwa kawaida na baada ya mwezi anatarajiwa kurudi uwanjani hivyo ataikosa mechi ya watani itakayochezwa Oktoba 18, Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za daktari wa Simba, Yassin Gembe, zimesema kiungo huyo hajapata majeraha makubwa lakini atakaa nje kwa muda huo ili kuwa imara zaidi.

 

Fraga aliumia dakika ya sita baada ya kukanyaga vibaya wakati akiwania mpira timu yake ilipocheza dhidi ya Biashara United ikiwa ni mchezo wa tatu wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo Simba ilishinda kwa mabao 4-0  na nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla..

 

“Atakosekana kwenye huo mchezo wa watani lakini Simba ina wachezaji wengi, ambao watacheza siku hiyo,” amesema Manara.

Leave A Reply