The House of Favourite Newspapers

Mbunge Abood Akabidhi Ambulance Hospital Ya Wilaya

0

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood amekabidhi gari ya kubebea wagonjwa (ambulance) hospitali ya wilaya Morogoro

Mbunge amesema atahakikisha wananchi wanapata huduma bora za kiafya hivyo ametoa Wito kwa wahuduna kuendelea kutoa huduma bora na kuahidi kuendelea kufikisha kwa Rais changamoto zilizopo katika sekta hiyo Ili zitatuliwe

Abood amesema Rais Samia Suluhu Hassani amekua akitoa Vifaa tiba pamoja kujenga vituo vya afya na zahanati Kila Kijiji lengo kuendelea kuboresha afya za wananchi wake

“gari hili niliomba Kwa Mhe. Rais hivyo kutokana na mapenzi yake kwetu sisi watu wa Morogoro ametupatia gari bila kusita tuna kila.sababu ya kumshukuru Kwa mapenzi yake ”

Amina Juma ni mmoja wa wananchi wa Mkundi Morogoro amesema kupatikana Kwa gari Hilo litasaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto

“tulikua tunapata shida Sanaa lakini sasa hivi mwaka Mtoto Mwaka mimba ahsante sanaa Mhe. Rais Samia”

Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiwemo wa Serikali,dini na vyama vya siasa.

Leave A Reply