Mbunge Aliyeiba mkate dukani Ajiuzulu

 

MBUNGE mmoja nchini Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu kama ”Sandwich” katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia.

 

Darij Krajcic ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa alipuuzwa na wafanyakazi wa duka hilo kwani walikuwa wakiendelea na shuguli zingine bila kumhudumia.

 

Hakujulikana kama ameiba mkate uliotajwa, lakini baadaye baadhi ya wateja walisisitiza arudi kulipia mkate huo. Krajcic ameomba msamaha na kusema kuwa anajutia kitendo alichokifanya.

 

Suala lake la kuiba lilisambaa baada ya habari kuwafikia wabunge wenzake wakati wa mkutano wa kamati siku ya Jumatano.

 

”Nilisimama pale kwa dakika tatu bila kuhudumiwa, ” mbunge huyo mwenye miaka 54 alisimulia kisa hicho katika kituo binafsi cha runinga.

 

Wafanyakazi watatu wa duka hilo hawakugundua kama mbunge huyo  alikuwa ndani ya duka hilo wakati wakiendelea na mazungumzo baina yao, hali iliyosabisha profesa huyo wa zamani kujaribu ‘bahati yake’.

 

”Hakuna mtu yoyote aliyepiga kelele, wala kunifuata,” aliwaambia wabunge wenzake waliocheka baada ya kusikia kisa hicho.

 

Lakini siku ya Alhamisi spika wa bunge hilo, Brane Golubovic, alikemea vikali kitendo cha mbunge kuiba, na kusema kuwa ni kitendo kisichokubalika.

 

”Amechukua hatua za kuwajibika na kujiuzulu yeye mwenyewe,” Golubovic aliviambia vyombo vya habari.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club


Loading...

Toa comment