The House of Favourite Newspapers

Mbunge CCM Afariki Baada ya Kugongwa na Trekta

0
Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM) Francis Leonard Mtega aliyesimama enzi za uhai wake.

MBUNGE wa Jimbo la Mbarali Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Fransis Leonard Mtega (CCM) jana Jumamosi alasiri amefariki dunia baada ya kupata ajali ya pikipiki aliyokuwa akiiendesha kuelekea shambani kwake, kugongwa na trekta aina ya Power Tiller.

Akitangaza kutokea kwa kifo hicho, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameeleza kusikitishwa na ajali hiyo na kutoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu jamaa, wabunge na wananchi wa jimbo la Mbarali.

Amesema ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaratibu mipango ya mazishi hivyo taarifa zaidi zitatolewa baadae.

Awali akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali mstaafu Denis Mwila ameyokea saa 9 alasiri baada ya pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili MC 573 CGY aliyokuwa akiendesha marehemu kugangana na ‘Powertilla.’

“Ajali hiyo imetokea kwenye barabara ya vumbi wakati marehemu akitokea shambani kwake akielekea Kata ya Chimala wilayani Mbarali ambako alikuwa akiishi.

“Tayari dereva wa ‘Powertilla’ Alex Musa (18) anashikiliwa na Polisi na chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva huyo ambaye hakuchukua tahadhari na kuendelea mwendo mbaya kwenye barabara ya vumbi jambo ambalo lilisababisha ajali hiyo.

“Tulishatoa tahadhari na masharti madereva wote wa ‘Powertilla’ ifikapo saa 12 jioni kutofanya kazi kutokana na madereva wake kutokuwa na leseni, lakini pia nyingi hazina taa zinazoweza kuonyesha usalama wawapo barabarani,” amesema.

Leave A Reply