Shigongo Afunguka Maajabu Ya Miaka 3 Ya Rais Samia Jimboni Buchosa – Video
Mbunge Eric Shigongo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maji, Ujenzi wa Visima 15 katika Jimbo la Buchosa ili kuepukana na Changamoto ya maji inayopelekea Wananchi kufariki kwa kuliwa na Mamba ziwani.
Pia mbunge huyo ameishukuru Serikali kwa Ujenzi wa Vizimba 4 ndani ya Jimbo hilo ambavyo vinatumika kwa ajili ya kujilinda na changamoto ya mamba inayosababishwa na Upungufu wa Maji ndani ya Jimbo la Buchosa.