The House of Favourite Newspapers

Mbunge Gambo Azungumza Na Rais Samia Kwenye Mkutano Mkubwa Na Wananchi, Atoa Maagizo – Video


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezungumza mbashara na walimu waliokusanyika katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani Oktoba 5, 2024 yanayofanyika Uwanja wa General Tyre mkoani Arusha, yakiwa yameratibiwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo ambapo amewapongeza kwa kuunga mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia ambayo yeye mwenyewe amekuwa akiipigia chapuo

Rais Samia amesema kuwa kutokana na jitihada hizo za walimu kwenye nishati safi, na yeye ameahidi kuongeza chochote ili walimu wakawe mabalozi wazuri wa nishati hiyo kwa wanafunzi na ndugu na jamaa zao.

Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha masilahi ya walimu kadiri muda na uchumi utakavyoruhusu.