The House of Favourite Newspapers

Mbunge: Hatukuungana Kugawana Umaskini, Zanzibar Iheshimike – Video

Mbunge wa Malindi, Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), amesema kwamba muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, haukuwa kwa lengo la kugawama umaskini bali kugawana faida kwa lengo la kila upande kufikia maendeleo ya kweli.

 

Saleh ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma ambapo amesema kwa kipindi kirefu, Wazanzibar wamekuwa wakizuiliwa kuleta biashara zao Bara, akitolea mfano wa Kampuni ya Simu ya Zantel kwamba ilizuiliwa kuja Bara kwa miaka mitano mpaka baadaye ikaanza kusuasua mpaka sasa.

 

Mbunge huyo amesema ipo haja ya watu wote kuanza kufikiri upya kuhusu umuhimu wa Zanzibar kwani kama itaendelea kupuuzwa, chuki itaendelea kuongezeka na kuwa bomu ambalo linaweza kulipuka muda wowote na kusababisha madhara makubwa.

Hatukuungana Kugawana Umaskini, Zanzibar Iheshimike -Ally Saleh

Comments are closed.