Mbunge Jaguar: Wachina, Watanzania Waondoke Kenya, Tutawapiga Mawe – Video

KENYA: Mbunge wa Jimbo la Starehe, Charles Njagua ‘Jaguar’,  amesema hataki kuwaona wafanyabiashara kutoka China, Tanzania na Uganda kwenye jimbo lake akidai kuwa wamekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wazawa wa nchi hiyo kukuza biashara zao kutokana na mashindano ya kibiashara baina yao.

 

Katika kipande cha video kinachosambaa mitandaoni, Jaguar ambaye pia ni mwanamuziki, amesema wanawapa saa 24 wafanyabiashara hao ambao ni raia wa nje (sio Wakenya) kuondoka nchini humo la sivyo watawapiga mawe na kwamba hawaogopi mtu wala kitu chochote.

 

Watanzania, Waganda na Wachina wanaofanya biashara Kenya, hatuwataki, hatutaki wafanyabiashara wetu wa-compete na wafanyabiashara wa nje, tunawapa masaa 24 waondoke. Tunaomba waziri na idara ya uhamiaji alishughulikie hili, wasipoondoka tutawapiga na hatuogopi mtu,” amesema Jaguar.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

 

Aidha, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemshutumu vikali Jaguar kwa kauli yake hiyo akidai kuwa inaweza kua na madhara makubwa kwa mshikamano wa mataifa hayo na mustaklabari wa watu wake.

 

 


Loading...

Toa comment