The House of Favourite Newspapers

Mbunge Janeth Mahawanga Alivyorejesha Matumaini Mapya Kwa Wajane

0
Mbunge Janeth Mahawanga (aliyesimama) akizungumza na kinamama wajane kwenye mkutano huo.
Dar es Salaam, 21 Septemba 2024: Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga amerejesha matumaini mapya kwa Wajane wa Mbagala Mwanamtoti Wilayani Temeke, Dar.
Mbunge Mahawanga alirejeshwa matumaini kwa kinamama hao wajane kwenye mkutano wao wa kuzindua kikundi chao cha kusaidiana kiitwacho UWANE uliofanyika jana (Jumamosi) Mtaa wa Sayari Kata ya Kijichi Mbagala Mwanamtoti jijini Dar.
Katika tukio hilo Mbunge Mahawanga alikuwa ndiye mgeni rasmi ambaye akizungumza na kinamama hao aliwapa mbinu mbalimbali za kukiboresha kikundi chao na kuwaahidi kuwaongoza kupata mkopo mkubwa wenye masharti nafuu na mafunzo ili waanzishe miradi itakayowakwamua kimaisha na kuondoa mkono shavuni kuomboleza na maisha ya ujane.
Mbunge Mahawanga aliwaeleza kinamama hao jinsi alivyowakomboa wenzao waliokuwa wakiishi kwa kazi ya kuponda kokote kwa nyundo na mikono yao maeneo ya Kunduchi na sasa wanaishi maisha bora baada ya kuwawezesha kupata maarifa na kuwaongoza kupata mkopo uliowawesha kununua mashine za kisasa za kuponda kokote na mpaka sasa ni wafanyabishara wakubwa wenye mashine za kuponda kokote na wana gari zao wenyewe za kusambaza kokoto kwa wateja wao.
Katika kikundi hicho pia walikuwepo walemavu wa macho wa aina mbalimbali ambao nao mpaka sasa wanalelewa na kikundi hicho na kuachana na kazi ngumu ya kuponda kokote kwa nyundo na mkono.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS/ GPL 
Leave A Reply