
MBUNGE wa Misungwi (CCM) na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema kama Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango anadai wizara yake haina fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali ni vyema akajiondoa katika wadhifa huo.
“Hivi kwanini unakosa fedha? Kama ni waziri wa fedha halafu unasema hakuna fedha ondoka hapo, kama wewe ni mbunge na kunamatatizo kwenye jimbo lako, ondoka,” alisema Kitwanga.
Kitwanga ametoa kauli hiyo jana Alhamisi, Mei 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati mwaka 2018/19. na kuishauri Serikali kuanzisha miradi ya kuzalisha umeme mkubwa badala ya miradi midogo.
“Miradi midogo ina gharama kubwa za uendeshaji, kila mradi unatakiwa iuwe na wataalam, meneja, na watumishi wengine, uwalipe mishahara, mimi nikushauri Waziri wa Nishati, mdogo wangu, Dk Medard Kalemani uje na mpango wa kuzalisha umeme wa Megawati 5,000 kwa kutumia makaa ya mawe,” amesema Kitwanga.


Comments are closed.