Mbunge Janeth Mahawanga Alivyowaongezea Maarifa Wanawake wa Tai Group Kata ya Pugu, Dar
Dar es Salaam, 27 Septemba 2024: Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga leo alizindua vikundi vinne vya kimaendeleo vya wanawake wa Kata Pugu Jimbo la Ukonga jijini ambavyo umoja wake unaitwa Tai Group.
Katika risala yao wanakikundi hao walielezea jinsi walivyopambana kuanzisha vikundi hivyo na kuelezea walipofikia na walipokwamia ambapo Mbunge Mahawanga aliwaelekeza jinsi ya kufanya na kuwapa mbinu za kufanikiwa kupata kiasi cha pesa wanazohitaji zaidi ya milioni ili waweze kuifanya biashara yao ya kuoka mikate kisasa zaidi.
Mbunge Mahawanga ndiye aliyewakwamua wanawake na walemavu waliokuwa wakiponda kokote kwa nyundo na mkono pale Mbuyuni Tegeta na sasa ni WAFANYABIASHARA wakubwa wenye magari yao na mashine za kisasa za kuponda kokoto.
Wiki iliyopita alizungumza na kinamama wajane wa Mbagala Mwanamtoti Kata ya Kijichi na kuwaelekeza jinsi ya kupata pesa za mkopo nafuu kutoka serikalini na tayari ameshaanza kupambania hilo.
Mama Lishe zaidi ya 100 wa Kata ya Mbezi Juu nao ni miongoni mwa walionufaika na Mbunge wao huyu wa Viti Maalum kwa kupatiwa mitungi ya gesi na kuondokana na matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa.