The House of Favourite Newspapers

Mbunge Nape Amuuliza Swali Gumu Waziri Mkuu Majaliwa Kuhusu Uchaguzi Serikali Za Mitaa – Video

0

ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amefika bungeni Jijini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa kwenye wadhifa huo Julai 21 mwaka huu.

Pamoja na kurejea Bungeni Nape ametumia kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu kumuuliza swali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ni lini Serikali itapitia upya msimamo wake wa mwaka 2016 wa kuzuia uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala kutokana na ongezekeo la watu kwenye mitaa, vitongoji na vijiji.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema ni kweli mahitaji ya uanzishwaji wa mamlaka hizo umekuwa ni mkubwa lakini Serikali inaangalia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha ili kuanzisha maeneo hayo mapya ya utawala.

Amesema kwa sasa kuna timu imeundwa ya kupitia maeneo mbalimbali ili kuona kama miundombinu ya kutolea huduma imekamilika na ikimpendeza Rais ambaye ndiye msimamizi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) atatangaza tena uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala nchini.

Leave A Reply