The House of Favourite Newspapers

Mbunge Salim Wa Ulanga Awataka TFS Kuwapa Elimu Bodaboda Ili Wasisumbuane

0
Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro, Mhe. Salim Alaudin Hasham Almas.

Morogoro 18 Mei 2023: Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro, Mhe. Salim Alaudin Hasham Almas amewaomba Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuachia pikipiki za vijana wa bodaboda walizozishikilia kwa kosa la ubebaji mkaa bila kibali kwani vijana hao hawakupewa elimu ya kutosha kuhusu namna bora ya kufanya biashara hiyo.

Baadhi ya madereva wa bodaboda na wamiliki wakimsikiliza kiumakini mbunge wao.

Akiongea mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Dkt. Julius Ningu, mbunge huyo amesema chanzo cha vijana hao kutenda kosa hilo kumetokana na TFS kutokuwa karibu na wafanyabiashara wa mazao ya misitu hivyo kupelekea watu kuvunja sheria pasipo kujua kwa kukosa elimu stahiki ya namna bora ya kufanya biashara hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dkt Ningu ametoa siku 10 kwa uongozi wa wakala wa huduma za misitu kuangalia namna bora ya kuwawezesha vijana hao elimu waweze kufanya biashara zao bila changamoto.

Zaidi ya pikipiki 30 zilishikiliwa kwa kosa hilo la kubeba mkaa bila kibali maalum na tayari pikipiki hizo zinafanyiwa utaratibu wa kurejeshwa kwa wamiliki pamoja na kupatiwa elimu ili kuepusha uvunjifu wa sheria kwa wakati mwingine. HABARI/PICHA NA MWAJUMA RAMBO/ GPL Morogoro

Leave A Reply