The House of Favourite Newspapers

Mbunge Shigongo Aongoza Maadhimisho ya Sherehe ya Simba Day Buchosa

0
Wanachama na wapenzi wa Simba SC Buchosa, wakiwa pamoja na Mbunge wao Jimbo hilo Eric Shigongo

SHEREHE za Simba Day zinaendelea katika maeneo mbalimbali nchini kuelekea kilele chake kitakachofanyika agosti nane mwaka huu katika uwanja wa mkapa dar es Salaam.

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amewaongoza wanachama na wapenzi wa Simba SC kufanya shughuli za kijamii ikiwemo usafi kama maadhimisho ya kuelekea Simba Day

Tawi la Simba Buchosa limeadhimisha sherehe hiyo Kwa kufanya shuhuli mbalimbali za Kijamii zilizohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo.

 

Akizungumzia na mashabiki wa Simba wa Jimbo hilo kwenye uwanja wa shule ya msingi Luchili Shigongo amewapongeza viongozi, wanachama na mashabiki wote wa Simba Buchosa Kwa kufanya jambo ambalo linaleta hamasa ya kukuza Michezo na kuijali jamii.

Shigongo amesema ameridhishwa na usajili wa Simba SC kwa msimu huu na anaamini kikosi hicho kitafanya vizuri katika michezo ya kimataifa na Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2022/2023

Shigongo ameongeza kuwa amefurahishwa na usajili uliofanywa Kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza hivi karibuni na anaamini Simba itafanya vizuri zaidi msimu ujao kwenye mashindano ya kimataifa na ligi kuu bara.

Leave A Reply