Shigongo: Ni Muhimu Wananchi Kushiriki Uchaguzi, Chagueni Viongozi Wenye Sifa – Video
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amewaagiza wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi bora na wenye sifa katika uchaguzi wa Serikali ndogo za Mtaa 2024.
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ndani ya kisiwa cha kome, kata ya Lugata hapo jana septemba 16, 2025.
Shigongo ameongezea zaidi kuwa ni muhimu wananchi kushiriki katika uchaguzi lakini pia kuhakikisha vijana wanakuwa kipaumbele kuhakikisha wanawania nafasi hizo.