Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile Afariki nchini India
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ametangaza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile, kilichotokea leo Novemba 27 nchini India alipokuwa anapatiwa matibabu.
Miezi michache iliyopita Dkt Faustine Ndugulile alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya duniani (WHO) Kanda ya Afrika.