SANCHI AFUNGUKA ANACHOKIPATA KWA MBWA WAKE

ANAMALIZA mwaka vizuri! Mwanamitindo mwenye umbo tata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameweka wazi kwamba, anashukuru anamaliza mwaka akiwa anaendelea na maisha yake vizuri huku madili yake ya biashara ya mbwa aina ya bull yakiendelea kumfanya atanue kinoma mjini.

 

Akibonga na Over Ze Weekend, Sanchi alisema kuwa watu wengi wamekuwa hawamuelewi anapokuwa akipiga picha na mbwa, lakini ni kwa vile hawajui mbwa hao wanampa madili kwa kiasi gani.

 

“Maisha yangu yanaenda kama kawaida kwa ajili tu ya hao mbwa wanaowaona kwenye ukurasa wangu wa Instagram. Mimi ni balozi wa biashara hiyo hivyo riziki yangu ya kila siku inapitia hapo,” alisema Sanchi.

Toa comment