The House of Favourite Newspapers

MBWEMBWE ZAMUAIBISHA WOLPER

Jacqueline Wolper Massawe

AIBU yake! Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe amekumbwa  na dhoruba ukumbini baada ya kuonesha mbwembwe za kuserebuka muziki juu ya meza kwa staili ya kusasambua kisha kuteleza na kuanguka ‘pwaaa’. Mbwembwe hizo zilizoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda zilimuaibisha Wolper kwenye ukumbi uliopo katika Ufukwe wa Jembe ni Jembe jijini hapa ambapo Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ ilikuwa ikifanya pati ya awali (pre-party) ya onesho lao la Wasafi Festival lililofanyika katika Uwanja wa CCM-Kirumba, juzi.

Katika tukio hilo, wakati watu wakipata kilaji, mastaa ambao walitarajiwa kufanya makamuzi kesho yake kwenye Wasafi Festival walikuwa wakitambulishwa. Ulipofika wakati wa Wolper, yeye aliamua kupanda juu ya meza kama wafanyavyo wanenguaji wa staili ya kusasambua. Akiwa juu ya meza, DJ aliweka Wimbo wa Kwangwaru ambapo Wolper aliendelea kuonesha umahiri wa kukicheza kwa kukata mauno baab’kubwa. Kwa bahati mbaya, wakati akiendelea kufanya yake, maskini mwanadada huyo mrembo alipiga mwereka matata na kuangukia kisogoni.

Hata hivyo, alisaidiwa kunyanyuka na mabaunsa na mashabiki waliokuwa karibu ambao walimuinua kisha wakamkagua na kubaini hakupata maumivu makali hivyo shoo yake ikaishia hapo. Baada ya kushuhudia tukio hilo, baadhi ya mashabiki walisikika wakisema, eti huenda mambo yaliyompata Mondi kule Sumbawanga yalitaka kujirudia kupitia kwa Wolper.

Hata hivyo, shabiki mwingine alisikika akikemea hali hiyo. Ijumaa Wikienda lilimfuata Wolper na kumpa pole ambapo alishukuru. Wasanii wengine walioonesha vionjo kwa mashabiki waliohudhuria pati hiyo ni pamoja na Chin Bees, Lavalava, Gigy Money na Dudubaya Konki Konki Konki Masta.

STORI: RICHARD BUKOS, MWANZA

Comments are closed.