The House of Favourite Newspapers

Mc Gregor Apoteza Bilioni 2 kwa kubeti

 

Mkali wa UFC kutoka nchini Ireland, Conor Mc Gregor, ameangukia pua katika ubashiri wake, ambapo Jumapili hii aliweka Dola za kimarekani 745,000 (Sh Bilioni 2), akibashiri kuwa Renan Ferreira angempinga Francis Nganou lakini badala yake Nganou alipata ushindi katika raundi ya kwanza tu ya mchezo.

MC Gregor anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Dola Milioni 200 za kimarekani ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 545 za kitanzania, alitangaza mwishoni mwa wiki kuwa anamuunga mkono Renan Ferreira na kuwa atashinda Kwa knock out (KO) dhidi ya Francis Nganou, lakini mchezo ulikuja na Matokeo ya kushangaza zaidi baada ya KO ya raundi ya kwanza Kwa Nganou.

Huku yeye mwenyewe akisema “”Ni biashara isiyo na huruma na mimi ni mtu asiye na huruma,” alieleza.

Si mara ya kwanza kwa mkali huyo wa UFC kubeti kwa kiasi kikubwa kwenye michezo ya kupigana, kwani McGregor aliwahi kubeti dola 500,000 kwa mpinzani wake wa zamani Nate Diaz kumshinda Jorge Masvidal katika pambano la ndondi, ambapo Katika tukio hilo, McGregor alijishindia fedha nyingi kutokana na dau lake kubwa.

Ngannou aliyeshinda Kwa knockout yake ya kushangaza dhidi ya Ferreira, na kuelekeza ushindi huo kwa mwanawe marehemu, Kobe.

“Nimepigana pambano hili tu kwa ajili yake, Nilikuwa nataka kupigana kwa ajili yake… Natumaini wanaweza kukumbuka jina lake, kwa sababu bila Kobe, tusingekuwa hapa usiku wa leo,” alisema Nganou kuhusu mwanawe aliyefariki mwezi April akiwa na umri wa miezi 15 baada ya kupata itilafu katika ubongo wake.