MC PILIPILI AFUNGUKA KILICHOMLIZA KWA MCHUMBA WAKE

Emmanuel Mathias ‘MC na Mchumba’ke, Philomena Thadei

DAR ES SALAAM: Baada ya hivi karibuni mchekeshaji maarufu Bongo, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ kumvisha pete ya uchumba, mchumba’ke, Philomena Thadei na kuangua kilio, mwenyewe ameibuka na kufichua kilichomliza.

 

MC Pilipili aliangua kilio cha aina yake wakati akimvisha pete mrembo huyo na kuzua gumzo la aina yake kwani imezoeleka kwenye zoezi kama hilo mara nyingi wanawake ndiyo huwa wanaangua vilio.

 

Kutokana na gumzo hilo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta MC Pilipili na kumuuliza kuhusiana na kuangua kwake kilio ambapo alieleza kuwa alilia kutokana na changamoto alizokuwa amezipitia kwenye masuala ya uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo.

Alisema hadi kufikia hatua hiyo ya kumvisha pete na binti huyo kukubali, halikuwa jambo rahisi bali alikumbana na ugumu hivyo alipoyakumbuka hayo, alijikuta machozi yakimtoka.

 

“Nimepata misukosuko mingi sana kwenye uhusiano ndiyo maana hadi machozi yamenitoka kwa furaha kwa kuwa nimefikia hatua nzuri, natarajia kuanza vikao vya maandalizi ya harusi hivi karibuni na vitakuwa vya muda mchache kwa kuwa ninataka kufanya haraka iwezekanavyo,” alisema MC Pilipili.

 

Kwa upande mwingine MC Pilipili alisema kuwa, ndoa yake itakayofanyika hivi karibuni inatarajiwa kuhudhuriwa na wageni waalikwa 2,000 ambapo wachekeshaji watakuwa ndiyo washehereshaji huku ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali hivyo itakuwa ni harusi ya aina yake

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

STORI: Zaina Malogo, Risasi Mchanganyiko

Loading...

Toa comment