Mc pilipili asaidia wenye njaa

20160125040833 MC Pilipili akiongea na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.

Na Mwandishi Wetu
MCHEKESHAJI maarufu, MC Pilipili ameamua kujitoa na kuwasaidia wananchi mbalimbali wenye mahitaji maalum mkoa wa Dodoma ambao wamekumbwa na tatizo la njaa.

Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa akirudisha fadhila mara kwa mara kwa jamii, amesema ameguswa kwa kiasi kikubwa na wananchi kukosa chakula hadi kufikia hatua ya kushindia uji wa ubuyu au kula wadudu, ndipo akaona awasaidie wakazi wa Kikuyu, Msalato na vijiji vya Kigwe na Kichangani vilivyoko wilayani Bahi.

20160125041009“Ni jukumu letu kurudisha kwa jamii kile Mungu alichotujalia. Nimeguswa ndiyo maana nikawasaidia ndugu zangu kuunga mkono juhudi za serikali. Niwasihi na wengine kufanya hivyo kadiri wanavyoweza,” alisema MC Pilipili.


Loading...

Toa comment