The House of Favourite Newspapers

MC Pilipili: Ben Pol atawakonga nyoyo Boxing Day

0

benpolMwandishi wetu

MKALI wa kuchekesha Bongo, MC Pilipili, amewataka wakazi wa Dodoma kukaa mkao wa burudani kwani anatarajia kufanya bonge la shoo la Stand Up Comedy ambapo Ben Pol naye atahusika kushusha burudani kali siku ya Boxing Day, Desemba 26, mwaka huu.

MC Pilipili amesema siku hiyo maalum ya kufungua zawadi, kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi kwa viti vya kawaida na shilingi elfu thelathini kwa viti maalum (V.I.P), watu watapata kumshuhudia live jukwaani katika Ukumbi wa Royal Village akionesha vibwanga vya hali ya juu vitakavyowafanya wavunjike mbavu kwani hana utani anapokuwa kazini.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde.

Leave A Reply