The House of Favourite Newspapers

Mc Pilipili,Ben Pol kufanya maajabu Boxing Day

0

benpol na pilipiliMC Pilipili akiwa na Ben Pol.

MWANDISHI WETU
MCHEKESHAJI maarufu Bongo, MC Pilipili anatarajia kufanya shoo baab’kubwa ya kuchekesha siku ya Boxing Day, Desemba 26, mwaka huu mjini Dodoma itakayofahamika kwa jina la Night Stand Up Comedy.

Akiizungumzia ‘event’ hiyo, MC Pilipili alisema kupitia kampuni yake ya Pilipili Events, watafanya shoo kubwa ya kuchekesha ambayo haijawahi kutokea Bongo hivyo mashabiki wa komedi na wapenda burudani kwa jumla, wafike kwa wingi siku hiyo katika Ukumbi wa Royal Village.

“Nitakuwa na Ben Pol, ataimba nyimbo zake wakati na mimi nikifanya yangu jukwaani. Shoo itaanza saa moja usiku hadi usiku sana. Kiingilio kitakuwa shilingi elfu kumi kwa viti vya kawaida na shilingi elfu thelathini kwa viti maalum (V.I.P),” alisema MC Pilipili.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde.

Leave A Reply