Mcameroon Ashangaa Djuma Kutimuliwa Simba

Mrundi, Masoud Djuma.

BAADA ya juzi Jumatatu uongozi wa Simba, kuthibitisha kuachana rasmi na aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrundi, Masoud Djuma, kocha wa zamani wa kikosi hicho, Mcameroon, Joseph Omog ameibuka na kusema kuwa ameshangazwa na uamuzi huo kwa kuwa haukuwa wa busara.

 

Simba imefikia uamuzi huo kufuatia madai ya kutokuwepo kwa maelewano kati ya Djuma na kocha mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems. Djuma ana­husishwa na African Lyon ya Rahim Zamunda na inadaiwa huenda akaibukia huko wiki chache zijazo.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Omog alisema kuwa kwa upande wake anaona Simba imefanya maamuzi ya kushangaza kwa kuamini jambo waliloambiwa na upande mmoja bila ya kuangalia umuhimu wa mtu waliyemuondoa.

 

“Binafsi naona ni jambo la kushangaza, Simba wamem­fukuza Djuma, tatizo lilikuwa nini mpaka wamechukua maamuzi hayo, kwangu Djuma alikuwa ni kama mtoto wangu ninayemlea na wala hatujawahi kukosana kwenye kazi, wakati mwingine kupishana mawazo ni kawaida lakini ninachokisikia kipo tofauti sana.

 

“Kwangu naona bado Simba ilikuwa inamuhitaji kwa kuwa ameshakaa nao na anajua kila kitu, sasa kwa hali hiyo sioni na­fasi ya wao kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuwa huyo mwalimu nimesi­kia tu ametoka Ubelgiji, simjui kabisa,” alisema Omog.

 

Ikumbukwe, Omog alifanya kazi na Djuma kwa kipindi kifupi kabla ya Mcameroon huyo ku­timuliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Loading...

Toa comment