Chama cha Mapinduzi (CCM), kimetoa maombi kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuyapuuza makosa madogo madogo yaliyowafanya wagombea wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kuenguliwa ili warejeshwe.
Akizungumza na Wahariri, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu amesema kumekuwa na mapingamizi mbalimbali ambayo yamewekwa kwa vyama vyote ikiwamo CCM lakini baadhi ya mambo madogo yanahitaji kupuuzwa.