Mchekeshaji Maarufu Wa Tiktok Atembelea Kwao Senegal, Alamba Dili Na UNICEF – Video

Khaby Lame, kijana mwenye asili ya Senegal na mchekeshaji maarufu zaidi duniani kwenye mtandao wa TikTok, ameteuliwa kuwa Balozi Mwema wa UNICEF. Lame, ambaye hajawahi kusema neno kwenye video zake zinazotazamwa na mamilioni ya watu duniani, alihutubia vijana wa Senegal siku ya Ijumaa Januari 31 2025 alipoteuliwa rasmi kwa nafasi hiyo.
Akiwa na umri wa miaka 24, Lame ana zaidi ya wafuasi milioni 162 kwenye TikTok. Umaarufu wake ulianza kupaa kupitia video zake za kuvutia zinazomwonyesha akitumia ishara badala ya maneno.