Mchengerwa: Mradi wa Bonde la Msimbazi Kusaida malengo ya ujenzi wa Uwanja wa Yanga
WAZIRI wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amesema Mafanikio ya leo ya Yanga, kuna watu walifanya kazi kubwa kuhakikisha klabu hii inatulia.
Pia Rais Samia ameagiza zaidi bilion 400 zielekezwe kwenye mradi wa bonde la msimbazi. Mradi huo utaisaida sana kwenye malengo ya ujenzi wa Uwanja wa Yanga. Katika eneo hilo litajengwa daraja bora na la kisasa. Mchakato wa mradi huo utaanza mara moja na mradi wa Yanga utakuwa sehemu ya mradi huo.
Waziri Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo leo Jumapili Juni 9, 2024 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) katika Mkutano Mkuu wa Yanga.
“Nawashukuru sana Young Africans SC kwa kunialika kwenye mkutano wenu huu mkuu. Ni heshima kujumuika nanyi ikiwa nyie ni Klabu yenye mafanikio makubwa sana. Nafikisha salamu za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa chachu kwenye maendeleo ya soka nchi hii” Mgeni Maalum Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)”
“Mafanikio ya leo ya Yanga, kuna watu walifanya kazi kubwa kuhakikisha klabu hii inatulia. Utulivu wa Yanga ndio maendeleo ya soka letu. Mafanikio ya Yanga leo ni kwa sababu ya Injinia Hersi na wenzake walifanya kazi kwa utulivu na weledi mkubwa. Hongera sana Injinia Hersi kwa kufanya Klabu ya kisasa zaidi. Uwekezaji uliofanywa kwenye klabu hii imekuwa chachu ya maendeleo ya soka Tanzania.”amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa