The House of Favourite Newspapers

Mchezaji wa Yanga, Ally Yusuf Amefariki Dunia Dar Leo

0

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Yusuf ‘Tigana’ amefariki dunia leo Novemba 5, 2019 Alhamis mchana katika hospitali ya Amana, Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa hospitali hapo.

 

Akithibisha kifo hicho, mchezaji Lubigisa Lubigisa alisema ni kweli Tigana amefariki leo mchana baada ya kuugua ghafla kuhara na kutapiki na kukimbizwa hospitali ya Amana ambako mauti yamemkuta.

 

Lubigisa alisema awali mke wa Tigana ndio alikuwa akiumwa na alikuwa amelazwa Amana, hivyo jana Jumatano alipokwenda kumuangalia hali ya mchezaji huyo ikaanza kubadilika.

 

“Alipofika nyumbani hali yake ikabadilika, akaanza kutapika na kuharisha kisha kukimbizwa hospitalini Amana, lakini baada ya kufika hapo alizidi kubadilika zaidi kutokana na kutapika akazidi kuishiwa nguvu,” alisema Lubuigisa.

 

Aliongeza kutokana na hali alizidi kupungua hadi mauti yalipomkuta mchezaji huyo.

Uongozi wa Yanga kupitia ukurasa wake wa Instagram umetoa pole kwa familia ya Tigana kwa kuandika. Uongozi wa klabu ya Yanga umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji wetu wa zamani Ally Yusuf ‘Tigana’ kilichotokea leo mchana.

Tigana aliichezea Yanga kwa vipindi viwili aliingia 1994-1995 na baadaye 2001-2004. Mungu ailaze roho ya maheremu mahali pema peponi amini.’

Leave A Reply