MCHUMBA AGOMA KUMZALIA BEN POL

Benard Paul ‘Ben Pol’na Anerlisa Muigai

 DAR ES SALAAM: Miezi michache baada ya kutambulishwa ukweni nchini Kenya, mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’, Anerlisa Muigai amegoma kumzalia jamaa huyo.  

 

Katika mahojiano yake na mitandao ya Kenya, Anerlisa (31) ambaye ni mjasiriamali mkubwa nchini humo akiwa anamiliki Kampuni ya Nero inayohusika na maji ya kunywa alisema kuwa, licha ya kupenda sana watoto, lakini linapokuja suala la kubeba ujauzito anaogopa na hayupo tayari kwa sasa.

“Mimi ni mmojawapo kati ya watu wanaopenda sana kuwabeba watoto wa rafiki zangu na kucheza nao. “Binafsi sijawahi kabisa kufikiria kuja kuwa mama labda taratibu huko mbeleni nitakuja kwa sababu mchumba wangu ameniambia kuwa ndoto yake ni kupata mtoto wa kike,” alisema mchumba huyo, kauli iliyotafsiriwa kuwa amemgomea.

 

Wawili hao waliingia rasmi kwenye uhusiano Aprili, mwaka jana ambapo mwishoni mwa mwaka walitangaza rasmi kuwa pamoja. Tayari ndugu wa pande zote wameshakutana Nairobi, Kenya na kinachosubiriwa ni ndoa.


Loading...

Toa comment