Mchumba wa Khashoggi Agoma Kuwasamehe Waliyomuua Mpenzi Wake

Mchumba wa Kituruki wa mwanahabari wa Saudi Arabia aliyeuawa kinyama Jamal Khashoggi, amesema leo kuwa hakuna mwenye haki ya kuwasamehe wauaji wa mwandishi huyo, baada ya watoto wake wa kiume kusema wamewasamehe wauaji.

 

Khashoggi, mtu wa karibu na familia ya kifalme aliegeuka mkosoaji, aliuawa na kisha mwili wake kutenganishwa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul nchini Uturuki, Oktoba 2018.

 

Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman alituhumiwa kwa kuamuru mauaji hayo, lakini serikali inaendelea kukanusha vikali tuhuma hizo.

 

Mchumba wake; Hatice Cengiz, amesema katika ujumbe wa Twitter kwamba mauaji ya Khashoggi hayana ukomo wa kisheria na hakuna mwenye haki kusamehe wauaji wake.


Loading...

Toa comment