MCHUMBA WA MOND ACHAFUKA UKWENI

BAADA ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutangaza tarehe ya kumuoa mrembo shombeshombe wa Mombasa nchini Kenya, Tanasha Donna Barbieri Oketch ‘Zahara Zaire’ ambayo ni Februari 14, mwakani, mrembo huyo amechafuka ukweni.

 

Risasi Mchanganyiko lilimshuhudia Tanasha akiwa sambamba na Diamond au Mondi walipotinga mjini Morogoro kwa ajili ya shoo ya Wasafi Festival iliyofanyika Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Jamhuri. Akiwa kiwanjani hapo, kila aliyeambiwa Tanasha ndiye mchumba ambaye Diamond ametangaza kumuoa alipigwa na butwaa.

 

KWA NINI?

Mrembo huyo alikuwa amevaa kihasara mno huku akiacha nje sehemu kubwa ya mwili wake hasa juu. Pia alishuhudiwa akiwa ameacha wazi kitovu chake mbele ya Watanzania maelfu waliojazana uwanjani hapo bila kujali kuwa yupo ukweni!

 

“Jamani…jamani! Huyu si ndiye Tanasha ambaye Diamond ametangaza kumuoa? Sasa mbona tumbo lote na kifua ameacha wazi utadhani yupo beach (ufukweni)? “Ona alivyojisitiri kidogo tu kifuani na kinguo chenyewe kinamvuka! Ina maana hakujua anakuja sehemu ambayo kuna wakwe zake? Ona sasa hii aibu anayoipata ukweni.

KWANI MORO NI UKWENI?

“Ukiacha notion (mtazamo) kwamba Tanzania ni ukweni kwake, lakini pia hapa Moro ndipo chimbuko la Diamond kwa hiyo ni ukweni kwake.

 

CHIMBUKO KIVIPI?

“Ukiacha upande wa Anko Shamte ambaye ni mume wa sasa wa mama Diamond (Sanura Kassim ‘Bi Sandra’) ambaye hapa Moro ni kwao, pia baba Diamond mwenyewe (Abdul Jumaa) hapa ndipo chimbuko lake.

“Muulize baba Diamond atawaambia kwamba hapa Moro ndipo lilipo chimbuko la familia yao. “Hivyo ni sahihi kabisa kusema kwamba kitendo alichokifanya Tanasha cha kuvaa kihasara ni kujichafulia sifa hapa ukweni,” alisema mmoja wa watu wa makamo aliyehudhuria shughuli hiyo na kumuona Tanasha alivyokuwa amevaa na kushindwa kujisitiri.

TANASHA NA MAMA DIAMOND

Bila kujali, Tanasha alipokutanishwa uso kwa uso na mamamkwe wake ambaye ni mama Diamond hakuonekana kushtuka alivyokuwa amevaa, bali alionesha ni jambo la kawaida. Hata hivyo, katika kuua ‘soo’, dada wa Diamond, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ndiye aliyekuwa beneti na mrembo huyo ili mama Diamond asipate nafasi ya kumhoji alivyokuwa amevaa.

MAMA DIAMOND ABADILI GIA ANGANI

Kufuatia utambulisho huo wa Tanasha kuwa mkwewe mpya ilihali mama Diamond alikuwa akijinasibu na mrembo mwingine aliyedaiwa kutoka na Diamond, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ kila mtu alitamani kujua msimamo wake kwa sasa.

Risasi Mchanganyiko lilimvaa mama Diamond kutaka kujua msimamo wake juu ya namna alivyompokea mrembo huyo ambapo katika hali ya sintofahamu aliamua kubadili gia angani. Awali, kulikuwa na taarifa za mama Diamond kumkataa mkwewe huyo kutoka Kenya, Tanasha kutokana na kumkubali Kim Nana.

Katika mahojiano maalum juu ya mapokeo yake juu ya Tanasha, mama Diamond alianza kwa kukanusha habari kuwa alimkataa mrembo huyo na kwamba alikuwa anamtaka Kim Nana. Mama Diamond alisema anamkubali Tanasha kwa moyo mmoja wala hana kipingamizi naye na ikitokea mwanaye kweli anataka kumuoa, basi yupo radhi wala hana shida.

“Sasa nimkatae amenikosea nini mtoto wa watu? Nani amesema mimi nimemkataa mkwe wangu? “Kama mwanangu amemuona anamfaa, basi nipo radhi amuoe maana umri unaenda na umri wa kuoa ndiyo huu. “Nimemkumbatia mkwe wangu kwa mapenzi yote, Mungu asaidie ndoa ifungwe. “Kwanza amekaa na nani pale (mama Diamond anahoji mtu aliyekuwa karibu na Tanasha uwanjani hapo)? Ngoja nikamuangalie,” alisema mama Diamond akielekea mahali alipokuwa amekaa Tanasha kwa ajili ya kujua ulinzi wake.

Alipoulizwa alichukuliaje alivyokuwa amevaa na kuacha sehemu kubwa ya mwili wake wakati yupo ukweni, mama Diamond hakutaka mazungumzo zaidi.

ESMA SASA

Kwa upande wake Esma ambaye alikuwa beneti na Tanasha alifunguka kuwa kwa upande wake alimpokea wifi yake mpya kwa mikono miwili.Esma ambaye amepachikwa jina la Yuda mitandaoni kutokana na kuwageuka warembo ambao huwa wanakuwa na Diamond kisha kupigwa kibuti alisema:

“Wala sina shida, nimemkubali wifi yangu na kwa sababu Nasibu (Diamond) mwenyewe ndiye amesema anamuoa na ameridhiana naye, mimi ni nani nikatae? “Kikubwa ninawaombea heri tu asiwe kama wengine ili na mimi nipate wifi wa halali, niache uyuda,” alisema Esma.

KIFUATACHO…

Baada ya shoo ya Morogoro kifuatacho kwa Wasafi Festival ni shoo ya kukata na shoka itakayofanyika Desemba 8 kisha Zanzibar Desemba 11 na Mwanza itakuwa Desemba 15.

Stori: SHAMUMA AWADHI NA MUSA MATEJA, MORO

 

FULL SHANGWE! Diamond Alivyopanda Stejini Morogoro!

Toa comment