The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Akutwa Akisali Uchi na Wanawake 7

MCHUNGAJI wa Kanisa la Full Gospel  na waumini wake ambao ni wanawake saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika wilaya ya Rukiga nchini Uganda kwa tuhuma za kukutwa wakisali huku wakiwa watupu ndani ya nyumba ya mmoja wao anayejulikana kwa jina la Adah Kahababo ambayo wamedai kuwa ndiyo kanisa lao.

 

Wakizungumzia tukio hilo, Kamishna wa Makazi wa Wilaya, Emmy Ngabirano na Mkuu wa Polisi wa eneo hilo John Mavure, wamesema  watu hao ambao ni wake za watu na kuwa wameshangazwa na kitendo hicho ambacho licha ya kuvunja maadili, pia ni jambo la kushangaza.

 

“Tunaheshimu uhuru wa kuabudu, lakini watu lazima wafuate utaratibu wa kuendesha kanisa.  Watu waliokamatwa walikuwa wanaendesha mkusanyiko kinyume na sheria, tena ndani ya nyumba ya mtu ambayo wamedai ni kanisa lao.  Sisi kama watu wa usalama hatuwezi kuliacha kwa sababu mwaka 2000 kuna watu walichomwa moto kanisani kwa tukio kama hili,” amesema Kamishna Ngabirano.

 

Hata hivyo, waume zao wamesema wake hao wameyakimbia makazi yao kwa takriban wiki sasa, na kwenda kuweka kambi kwa Bi. Kahabado kwa ajili ya maombi ya usiku na mchana.

 

Waliokamatwa ni Mch. Aggrey Elias Mubangizi wa Manispaa ya Ibanda, Adah Kahabado, Christina Arinda, Hope Nyamurungi, Apohia Tumusiime, Anna Mugabirwe, Angela Nyangoma na Moreen Nyangoma, wote wakazi wa Rukiga.

VITUKO USWAHILINI: Anaswa akichungulia watu waki…!!!

Comments are closed.