The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Aliyefufua ‘Maiti’ Azua Gumzo – Video

NI Jumapili asubuhi ambapo kuna ibada ya uponyaji katika kanisa la  Alleluia Ministries International, kaskazini mwa jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, likiongozwa na Mchungaji Pastor Alph Lukau. 

 

Watu waliofika hapo wakitumia viti vya magurudumu wanainuka na kutembea na waliokuwa wakitumia magongo ya kutembelea wanayatupilia mbali na kuanza kukimbia.  Hata  hivyo, bado kuna tukio kubwa zaidi litatokea.

 

Mara gari la kubebea majeneza linawasili likuwa na jamaa wanaolia kwa kuomboleza.  Lukau anaitwa na waombolezaji nje ya kanisa ambapo wanamwambia wamemleta ndugu yao aliyefariki tangu Ijumaa.  Dakika chache baadaye, huku maelfu ya watu wakitazama,  jeneza linafunguliwa na Lukau anamwekea mikono mtu huyo anayesemekana amekufa aitwaye Elliot.  Baada ya kumwombea kwa muda mfupi, mtu huyo anafufuka!

Umati wa watu uliopo na familia ya Elliot wanapigwa butwaa na muujiza huo uliotokea mchana kweupe na tukio hilo linawekwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo wasomaji wanashangazwa na kitendo hicho kinachodaiwa kuwa cha Mungu kupitia ‘mtu wa Mungu’.

 

Panasambaa fikra kwamba huenda mtu huyo angeweza kuwafufua marehemu Nelson Mandela, Hector Peterson, Hugh Masekela, Steve Biko, OR Tambo na wengine. Hata hivyo, panakuwepo maswali mbalimbali kama: Je, kitendo hicho ni cha kweli?

 

Kwa nini mfu huyo hakuonekana kama kweli alikufa siku mbili zilizopita?  Je, hati ya kifo iko wapi?  Kwa nini huduma hiyo haikufanywa na mtaalam wa masuala ya afya? Inavyoonekana kampuni ya mazishi iliyoleta jeneza hilo kanisani iitwayo Kings and Queens Funerals, ilihusishwa katika utapeli huo.

UTATA WA MCHUNGAJI LUKAU

Pamoja na yote hayo, Lukau ni mtu ambaye amekuwa akiendesha mambo yenye utata kila mara. Mwaka 2016 alitayarisha hafla kweye kituo cha  Gallagher Conference Centre alikowakaribisha maelfu ya wanawake waliotalikiwa akawaombea ili waolewe.

 

Hata hivyo, wanawake hao walibidi kulipa tiketi za (Rand) R450,  kuingia katika kituo hicho, na R5,000 kwa viti maalum.  Kilichotokea ni kwamba Jumapili iliyofuata, palifanyika hafla ya ndoa nyingi za pamoja ambapo wanawake hao walikuwa wamepata wanaume wa kuwaoa.

Isitoshe, Lukau pia hudai ana uwezo wa kutibu VVU/Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengine. Pamoja na yote hayo, Lukau hajafunguliwa mashtaka yoyote ya jinai au kuifikishwa mbele ya tume ya kuendeleza na kulinda haki za kiutamaduni na kidini (CRL)  ya nchini humo.

Lukau pia ameongeza utata wake kwa watu kwa madai ya kuponyesha VVU/Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengine.

Hata hivyo, mchungaji huyo amejikuta akipambana na mwandishi wa habari wa Nigeria anayefanya kazi nchini Afrika Kusini,  Solomon Ashoms, ambaye alimwita mchungaji feki kupitia akaunti yake ya  Facebook. Wakati hayo yakitokea, Lukau na kanisa lake hawajajibu hadharani mabai kwamba muujiza huo wa uponyaji ulikuwa umepangwa.

 

#GlobalHabariUpdates

 

View this post on Instagram

 

Unaamini huu muujiza?

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.