MCHUNGAJI ATABIRI JUU YA WAZIRI MKUU MSTAAFU 2019, ANENA MAZITO KUHUSU TAIFA – VIDEO

MTUMISHI wa Mungu, Pastor Malachi Joseph amewashangaza wengi baada ya kutoa unabii juu ya roho ya mauti kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Mchungaji amepewa maono hayo na Mungu na alionyeshwa Waziri huyo mkuu akipunga mkono ikiashiria kuaga dunia mwaka huu 2019.

 

Pastor Malachi ametoa utabiri huo katika ibaada maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania na kulikabidhi katika mikono ya Mungu iliyofanyika usiku wa Desemba 31, 2018, kwenye mkesha wa kuukaribisha, mwaka mpya 2019, katika Kanisa hi lililopo Kigogo, jijini Dar es Salaam mkabala na Kituo cha Polisi Kigogo na kusema;

 

“Sikiliza ambacho Mungu anakisema kuhusu Taifa, nabii hizi siyo kwa ajili ya kuleta hofu katika mioyo yetu, Mungu anafunua ili tuone, kama unanisikia tuungane katika kuomba ili Kuzuia yasitokee. Aliongoza maombi ya kumuombea Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ninamuona akipunga mkono, hiyo inaonyesha, kwaheri, maana yake kuna mauti,” alisema Pastor Malachi.

 

 

Baada ya kutoa nabii hiyo, Pastor Malachi ambaye amekuwa maarufu kwa kutoa mapepo, kuharibu nguvu za giza zilizokufunga, magonjwa sugu kama kisukari na presha, aliwaongoza waumini wote katika kumuombea Waziri Mkuu Mstaafu huyo ili mwenyezi Mungu amuepushe na kifo.

 

Kutazama Video yote ya Utabiri huo na maombezi, ingia kwenye YouTube channel ya Pastor Malachi J. Ministries au Bofya hapa ====> Pastor Malachi J. Ministries

Loading...

Toa comment