The House of Favourite Newspapers

MCHUNGAJI ATAFUNWA NA MAMBA AKIBATIZA ZIWANI

 

MCHUNGAJI ambaye aliyekuwa akiendesha ibaada ya kubatiza waumini ufukweni mwa ziwa amefariki baada ya kushambuliwa na mamba wakati akibatiza Kusini mwa Ethiopia.

 

Mchungaji huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Docho Eshete alikuwa akiendesha ibaada hiyo ya waumini 80 siku ya Jumapili iliyopita katika ufukwe wa Ziwa Abaya katika mji wa Arba Minch wilaya ya Merkeb Tabya.

 

Wakazi wa mji huo waliliambia shirika la utangazaji la BBC kwamba Mamba huyo aliruka kutoka ndani ya maji wakati mchungaji huyo akiwabatiza waumini na kumng’ata miguu,mgongo na mikono majeraha yaliyosababisha kifo chake.

Comments are closed.