The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Atembezewa Kichapo na Waumini, Awekwa Kitimoto

2

Mchungaji (1)Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ebenezer Mission lililopo Kisanga jijini Dar, Musa Mlezi (aliyeinua mkono akiashiriria kunena jambo).

Gladness Mallya na Hamida Hassan

Baada ya hivi karibuni Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ebenezer Mission lililopo Kisanga jijini Dar, Musa Mlezi kula kichapo kutoka kwa waumini wake kisa kikiwa ni madai ya kuoa wake wawili, mtumishi huyo wa Mungu juzikati aliwekwa kiti moto ili kutafuta muafaka.

Mchungaji (6)Kikao kikiendelea katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisanga

Kikao hicho kilifanyika Jumanne iliyopita kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisanga ambapo kiliongozwa na mwenyekiti wa eneo hilo, Enock Kaise Mayaha na kuhudhuriwa na waumini pamoja na viongozi wengine wa kanisa.

Mchungaji (3)Wajumbe wa kikao wakichangia maoni yao.

Katika kikao hicho, awali waumini walitoa dukuduku lao kwamba mchungaji wao amevunja sheria za neno la Mungu kwa kuoa mke wa pili hivyo walimtaka kuacha utumishi wake na kuwa muumini wa kawaida.

“Sisi tunataka aache uchungaji na awe muumini wa kawaida maana amekiuka taratibu za utumishi kwani ana mke na watoto watatu lakini ameoa tena mke wa pili.

Mchungaji (5)Kanisa la Pentekoste Ebenezer Mission lililopo Kisanga jijini Dar

“Hatutaki kulitukana jina la Mungu wetu hivyo akubali tu kuachia nafasi aliyonayo ili awepo mchungaji mwingine wa kutuongoza katika kanisa letu,” alisema mmoja wa waumini hao huku akiungwa mkono na wenzake.

Naye mchungaji alipotakiwa kujitetea alisema waumini hao wamemgeuka kwani mwanzo walikubali aoe lakini anawashangaa sasa hivi kumdhalilisha.
“Yule mke wa kwanza tuliachana tukiwa na watoto watatu ambapo ninaishi na wawili na yeye amebaki na mmoja huko Iringa.

Mchungaji (4)“Talaka ilishatoka tangu mwaka 2010 naye ndiye aliyeiomba, nimevumilia kwa miaka yote hiyo sasa nimeoa Desemba 27, mwaka jana na ndipo chokochoko zikaanza, nahisi kuna kitu nyuma ya pazia kwa hawa waumini,” alisema mchungaji huyo.

Mchungaji (7)Naye katibu wa kanisa hilo aliyetajwa kwa jina moja la Grace, alisema ameumizwa sana na kitendo hicho cha mchungaji kupigwa kwani ni laana na hakubaliani na madai ya waumini hao.

Mchungaji (8)Hata hivyo, kikao hicho kilivunjika baada ya kutopatikana muafaka ila wajumbe wakakubaliana kukutana tena siku nyingine kutafuta suluhu.

2 Comments
  1. asante says

    hukumu za kiroho hazitafutwi kwa waumini,hilo wangemuachia Mungu atajua yupi wakubaki yupi wa kwenda.

  2. Alex solomon says

    Mchungaji kachemka!

Leave A Reply