Askofu Gwajima Apata Pigo

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo jijiji Dar es Salaam, Josephat Gwajima jana Jumapili, Januari 21, 2018 alipata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi Bi. Ruth Basondole Gwajima ambaye aliriki dunia asubuhi.

 

Bi. Ruth Basondole Gwajima amefariki akiwa na umri wa miaka 84 na mazishi yake yatafanyika siku ya Alhamisi ya Januari 25, 2018, Salasala jijini Dar es Salaama.

 

“Leo (jana) Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018; Salasala Dar es Salaam” alisema Gwajima.

 

Toa comment