The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Hananja: Tusilaumiane kwa Mambo ya Dini au Kabila

0
Mchungaji Richard Hananja

MCHUNGAJI Mstaafu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Richard Hananja ametoa rai kwa wananchi kutobaguana au kulaumiana kwa tofauti ya dini au kabila kwani ni vitu ambavyo kila mtu alizaliwa akavikuta hakupanga.

 

Mchungaji Hananja ameyasema hayo leo katika kipindi cha HOTPOT kinachorushwa na Studio za Global TV na 255Global Radio wakati akijibu swali linalohusu kolabo ya Omoyo Remix iliyoimbwa na Harmonize pamoja na Jane Misso ambapo wadau wengi wa muziki waliweza kuhoji kwanini Harmonize muumini wa dini ya Kiislamu ameweza kuimba nyimbo yenye mahadhi ya dini ya Kikristo.

Nyimbo ya Harmonize na Jane Misso

“Dini isitufanye kufarakanishwa sisi wote thamani yetu ni moja, sisi ni wanadamu machoni kwa mungu hivi vitu ambavyo tumepewa duniani visilete shida ndiyo maana vitu muhimu vyote ameshika mungu, Usingizi ameshika mungu.” Amesema Mchungaji Hananja.

 

Mchungaji huyo ameendelea kwa kusema kuwa mbele ya mungu wanadamu wote wana thamani moja ndiyo maana hadi hewa tunavuta bure.

Mchungaji Hananja ndani ya Studio za Global TV na 255Global Radio

Aidha Mchungaji Hananja amebainisha kuwa ndoa nyingi zina matatizo na wanandoa wengi wanagombana kutokana na kuwa na tabia za umri na njia pekee ya kutatua matatizo hayo ni kupata majibu ya maswali kupitia maombi na imani.

Leave A Reply