The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Jela Miaka 30

1

Mchungaji huyo akiwa chini ya ulinzi pamoja na wenzake.

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa

UHALIFU! Mchungaji kutoka Nigeria, Chid Okechukwi aliyekamatwa na kikosi kazi (task force) cha kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya nchini akiwa na kilo 81 za madawa ya kulevya aina ya cocaine amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na faini ya shilingi bilioni tisa akitoka mwaka 2045.

Mchungaji Okechukwi wa kanisa moja la kiroho nchi humo alikamatwa Machi 12, 2013 maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiishi.

Taarifa kutoka vyanzo vyetu makini na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Diswalo Mganga zinasema mchungaji huyo alihukumiwa Ijumaa ya wiki iliyopita na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Huruma.

Mkurugenzi wa mashtaka katika mahojiano na Uwazi kwa njia ya simu juzi, alisema mchungaji huyo alihukumiwa na wenzake watatu ambao alikamatwa nao siku moja.Aliwataja wengine watatu kuwa ni Hycenth Stani (raia wa Afrika Kusini), Paul Ukechuwi (raia wa Nigeria) na Shoaib Mohammed (raia wa Pakstan), wote walikutwa katika nyumba hiyo inayodaiwa kuwa ni ya kigogo mmoja nchini.

Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, ACP Godfrey Nzowa alipohojiwa na Uwazi ofisini kwake jijini Dar wiki iliyopita, alisema anakubaliana na kasi ya mahakama kuu katika kuendesha kesi za madawa ya kulevya.

“Nimeshuhudia kesi nyingi za zamani zinazohusiana na madawa ya kulevya zimetolewa hukumu na wahusika wamefungwa kwa waliopatikana na hatia. Kasi hii ni nzuri, napongeza mahakama,” alisema Nzowa.
Kesi za kukutwa na madawa ya kulevya kwa sasa zimepamba moto ambapo hivi karibuni, Fred William Chonde alihukumiwa kwenda jela miaka 20 na faini ya shilingi bilioni 15 akitoka mwaka 2035.

1 Comment
  1. […] Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, ACP Godfrey Nzowa alipohojiwa na Uwazi ofisini kwake jijini Dar wiki iliyopita, alisema anakubaliana na kasi ya mahakama kuu katika kuendesha kesi za madawa ya kulevya. “Nimeshuhudia kesi nyingi za zamani zinazohusiana na madawa ya kulevya zimetolewa hukumu na wahusika wamefungwa kwa waliopatikana na hatia. Kasi hii ni nzuri, napongeza mahakama,” alisema Nzowa. Kesi za kukutwa na madawa ya kulevya kwa sasa zimepamba moto ambapo hivi karibuni, Fred William Chonde alihukumiwa kwenda jela miaka 20 na faini ya shilingi bilioni 15 akitoka mwaka 2035. CHANZO CHA HABARI NI globalpublishers. […]

Leave A Reply