The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Mgogo kuwafunda wana-Ndoa Mwanza

0

MCHANGAJI maarufu hapa nchini Daniel Mgogo anatarajia kuwafunda wanandoa na washiriki wa Mwanza Couple Night Gala kwa lengo la kuimarisha ndoa kiimani kutokana na Uwepo kwa mifarakano ya wanandoahali inayopelekea  kuwaacha watoto wadogo  katika changamoto za kukua bila malezi bora ya wazazi.

Hayo yameelezwa na Mwaandaji wa Warsha hiyo Betty Kwibisa na kusema kuwa warsha hiyo inatarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu katika Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza, tofauti na mafundisho ya kiimani lakini pia kutakuwa na maelezo ya kisheria kwa wanandoa  ambapo washiriki watapata kushiriki katika elimu ya mirathi ili kujua umuhimu wa kuandika wosia mapema ili kuepusha migongano ya kifamilia pindi inapotokea haupo Duniani.

Kutokana uwepo wa magonjwa yasiyoambukiza Daktari Bingwa atawapitisha washiriki katika njia sahihi ya kupima na kujua afya yao namna ya kufanya mazoezi. “kwa kuwa watu watakuwa na wenzi wao lazima watu wafurahi na wapate elimu  amesititiza wanandoa na wanatakiwa  kuingia kwa wingi kuhudhuliwa warsha hiyo  muhimu kwani inaenda kufungua akili yao.

Leave A Reply