The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Mwakipesile Ahukumiwa Kifungo Cha Miaka Mitatu Jela

0
Mbarikiwa Mwakipesile

Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani Tu”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha Huduma ya Kiroho bila kibali

Akizungumza na JamiForums, Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha. Pia, Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa.”
Ameongeza “Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini. Tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023).”

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUHUSU MTOTO WARDA – MAMA MZAZI AFICHUA MENGINE | MAPITO

Leave A Reply