The House of Favourite Newspapers

MCHUNGAJI TAJIRI WA KUTISHA MWENYE KANISA BONGO

Shepherd Bushiri.

UKIFIKA jijini Dar Es Salaam eneo la Makongo Juu ndipo lilipo kanisa la En­lightened Christian Gathering ‘ECG’ la Mchungaji Shepherd Bushiri.  Waandishi wengi duniani katika makala zao wamekuwa wakieleza kwamba utajiri mkubwa alionao Mchungaji Bushiri ni zaidi ya kinywa kinavyoweza kuelezea, zaidi ya fikra zinavyoweza kuwaza na zaidi ya mikono inavyoweza kuandika.

Bushiri maarufu pia kama Major 1 kwa mujibu wa Mtandao wa Indapaper.com kwa mwaka 2018 amekuwa mchungaji wa kwanza tajiri Afrika akimiliki kiasi cha dola 170 (Tsh 389 bilioni) zaidi ya dola milioni 20 (Tsh 45 bilioni) alizokuwa nazo miaka miwili iliyopita. Pengine ndiyo kusakafia maneno ya waandishi wengi kama nilivyosema kwamba Major 1 utajiri wake hauelezeki kwani hata takwimu kutoka chanzo kimoja kwenda kingine zinatofau­tiana.

Lakini itoshe kusema Bushiri ni miongoni mwa wachungaji mata­jiri zaidi siyo tu Afrika bali duniani. Bushiri ameweza kujikusanyia utajiri huo mkubwa akiwa na miaka 40. Swali: Amewezaje kupata mali katika umri huo? Bila shaka kurejea historia ya Bushiri linaweza kuwa jambo la kwanza ambapo mchungaji huyo anatajwa kuwa ni raia wa Malawi baba yake mzazi ni Eubert Angel kutoka Zimbabwe.

Ni mtoto wa sita katika familia yake, amesoma shule ya Sekond­ari Moyale. Baadaye akajiunga na Chuo cha Therapon ambako alichukua Shahada ya Uzamivu ya masuala ya Filosofia.

Kwa kuwa historia ya maisha ya Bushiri haifiki haraka kwenye uk­wasi alionao, mwenyewe amepata kueleza kwamba tangu akiwa mdogo aliitwa na Mungu kumtu­mikia, huko ndiko kulikochomoza mafanikio yote aliyonayo.

Inaelezwa asili ya jina lake ilitokana na mkasa aliokutana nao mama yake wakati akijifungua. Akiwa wodini madaktari walimwe­za kuwa kutokana na mazingira yaliyokuwepo asingeweza kujifun­gua kwa njia ya kawaida. Alihitaji kufanyiwa upasuaji, yeye alikataa. Walichokifanya madaktari ni kusubiri matokeo, kwamba mtoto, mama au wote wawili wapoteze maisha.

Hata hivyo matarajio yao hayakuwa. Walipotoka wodini alikokuwa amelazwa mama huyo, alijifungua salama, jambo hilo liliwashangaza madaktari. Kauli aliyoitoa mama huyo baada ya kujifungua ilikuwa ni: My God is my shepherd. Aki­maanisha Mungu ndiye mchungaji wangu.

Hapo ndipo lilipotoka jina la Shepherd Bushiri. Tangu kuza­liwa kwa Bushiri simulizi nyingi zimetokea. Inase­mekana akiwa na umri wa miaka mitano, Bushiri alitokewa na mtu anayemtaja kama Nabii Yesu aliyem­kabidhi Biblia na kumwambia kuwa anataka aifanye kazi ya kuhubiri.

Licha ya kwamba kazi ya kuhubiri aliianza mwaka 2002 lakini 2009 ndipo alipofungua kituo cha Uinjilisti katika Mji wa Mzuzu akifanya ma­hubiri yake chini ya mti.Related image

Kipindi hicho hakuwa tajiri, kitu kilichompa umaarufu ilikuwa ni karama ya kuponya wagonjwa. Huduma ya Bushiri ilizidi kukua; watu kutoka mataifa mbalimbali walifika nchini Malawi kufuata maombezi, ushuhuda wa uponyaji ulikuwa mwingi miongoni mwa wagonjwa.

Idadi ya waumini haikuchelewa kufika 50,000 katika kipindi kifupi. Hapo ndipo mchungaji Bushiri alipoibuka na hoja kwamba kuna baadhi watu hawampendi nchini kwake. Akakosoa mfumo wa uwekezaji wa Malawi na kuiita nchi isiyofaa kufanyia biashara.

Kwa ujasiri alitupilia mbali kauli za maadui zake waliokuwa wakim­tuhumu kuwa anatumia nguvu za giza katika kazi yake ya kuhu­biri huku wakiponda uwezo wake wa kuponya ugonjwa wa Ukimwi.

Yeye akasema hakuanzisha kanisa kwa ajili ya watu wote bali kwa waaminio. Wakati huo, tayari alikuwa ameanza kutanua huduma yake ambapo alifungua tawi la ECG katika Mji wa Pretoria nchini Afrika Kusini. Kama mti kwenye maji huko nako huduma ilishika mizizi haraka, waumini takriban 150,000 walikuwa wakihudhuria mahubiri yake.

Bushiri ambaye anajiita mtu wa Mungu akazidi kunawili kihuduma. Lakini kubwa likawa ni utajiri uliochipuka sambamba na kazi yake ya kueneza dini. Wengi hawaamini hata leo, kuwa dini inaweza kumfanya mtu kuwa tajiri kwa kiwango cha Bushiri, lakini mwenyewe ukimuuliza anasema pia ni Mfanyabiashara.

Major 1, baba wa watoto waw­ili aliyemuoa Mary Zgambo Julai 31, 2011 na harusi yao kufanyia katika uwanja wa mpira, hivi sasa ni muwekezaji mkubwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Dubai na Afrika Kusini.

Vyanzo vya mapato vina­vyoonekana katika historia yake ni umiliki wa Chuo Kikuu cha Kilimo, uwekezaji katika Nyanja ya mawasiliano, umiliki wa migodi ya dhahabu na Uinjilisti ambao ameujengea matawi katika nchi ya Tanzania, Afrika Kusini, Botswana na Namibia.

Kutokana na ukwasi alionao mchungaji huyu anamiliki ndege nne binafsi, magari ya kifahari yasiyokuwa na idadi, nyumba za kisasa huku maisha yake yakiwa ni ya kifahari. Jambo hili limekuwa likikuna vichwa vya wengi kwamba vipi dini inaweza kuwa chanzo cha utajiri wa kutisha wa baadhi ya wahubiri duniani.

Imani ya wengi imekuwa nyuma ya fikra pengine zinaweza kuwa potofu au la, kwamba huenda mbali na dini, baadhi ya wachungaji wanafanya biashara nyingine haramu kwa ajili ya kujiongezea kipato. Mara kadhaa baadhi ya wa­chungaji wamekuwa wakitiwa mbaroni na vyombo vya usalama katika nchi mbalimbali duniani wakituhumiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Kama hilo halitoshi, tuhuma nyingine zinazoelekezwa kwa baadhi ya wachungaji ni kutumia karama za uponyaji kujipatia fedha ambapo hivi sasa baadhi yao wamekuwa wakitajwa kuwa­fanyia maombezi wagonjwa kwa malipo fedha, jambo linaloelezwa na baadhi ya waumini kuwa dini imegeuzwa kuwa biashara.Image result for shepherd bushiri house

Hata hivyo, utetezi wa wachun­gaji wengi kuhusu wao kujilim­bikizia mali kupitia dini umekuwa ni kwenye maandiko kitabu cha 1Wakorinto 9:9 imeandikwa: Usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka. Tafsiri ni kwamba wao wa­naruhusiwa kula kwenye kile wanachokivuna kwa maana sadaka na michango kutoka kwa waumini wao.

Tangu kufunguliwa kwa Tawi la ECG nchini, kanisa hilo lime­kuwa likifikiwa na waumini wengi hasa wanaofuata maombezi. Mbali na Bushiri wachungaji wengine Wanaotajwa kuwa na utajiri usiokuwa wa kawaida ni pamoja na Chris Okotie, Matthew Ashimolowo, Temitope Joshua ‘TB Joshua’ wote hawa kutoka Nigeria.

MAKALA: RICHARD MANYOTA

Comments are closed.