The House of Favourite Newspapers

Mdee Apinga Msimamo wa JPM Kuhusu Waliopigwa Mimba Kutoruhusiwa Kurudi Shule

0

 

Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam (Chadema), Halima James Mdee amepinga kauli na msimamo wa Rais Dkt. John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Pwani kuhusu agizo la wanafunzi wanapopata mimba na kujifungua wasiruhusiwe kurudi shule kusoma.

 

Mdee ameupinga msimamo huo huku akimtaka rais afuate sheria na katiba ya nchi inayowaruhusu watoto hao warudi shule baada ya kujifungua.

 

 

Aidha, Mdee amesema kuwa anashangazwa na Waziri wa Afya, Dkt. Ummy Mwalimu ambaye amesema agizo hilo kuwa lisiendelee kuzungumziwa wakati wanaoumia ni watototo wenyewe ama kwa kubakwa na kusababishiwa ujauzito na hivyo ya Ummy inawanyima haki watoto kuendelea na masomo.

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Akina Rugemalila, Malinzi na Wenzake Kortini, Lissu Atoa Neno Kuachiwa kwa Aliyeshtakiwa kwa Makosa ya Mtandao

Leave A Reply