The House of Favourite Newspapers

NEW: Mdee Music Presents; MIMI MARS – SHUGA (Official Music Video).

Mwaka 2017 umeanza na sura na sounds mpya kwenye game ya Bongo Fleva. Baada ya kushuhudia video launch yake pale Club Next Door siku chache zilizopita, Mdee Music inaisogeza kwetu official music video ya SHUGA ya kwake Mimi Mars.

Ujio wa Mimi Mars kwenye game umeleta shauku kubwa kujua ni namna gani ataitofautisha sanaa yake na ile dada yake Vanessa Mdee kwani wapo tayari wanaodai kuwa ‘kisauti’ wawili hao hawajofautiana sana.

Kwa upande wa shemeji mtu JUX yeye anasema Mars sio wa kumchukulia poa kwani uwezo wake unaweza kuwa wa kumzidi dada yake Vee Money

Nimepata bahati ya kuwa na Mars kwa ukaribu kidogo, na naamini ana kitu kwa sababu kabla sijawahi kumuona Mars akiimba nilkuwa naambiwa na Vanessa kuwa unajua Mars anaimba sana lakini sikutake it serious kwamba eti anaimba sana, ila kuna siku nilisikizishwa wimbo wake wa zamani sana nikaona kuwa ana kitu alafu nikagundua kuwa anaweza akawa anaimba kuliko hata Vee…“- Jux alisikika akisema kwenye XXL ya Clouds FM.

Whether Mimi Mars ana uwezo mkubwa kushinda Vanessa au la ni mapema sana kusema kwa sasa ila kazi zake na ufikishaji wa sanaa yake ndio itakayomtofautisha yeye na dada yake kwenye soko zima la Bongo Flevani. Kwa sasa tuipokee kazi yake ya kwanza tuisikilize na tuitazame mara nyingi tuwezavyo kupitia YouTube.

MIMI MARS – SHUGA (Official Music Video).

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Comments are closed.