MDH Yaibuka Mshindi wa Pili Tuzo za NBAA 2024

MDH imeibuka mshindi wa pili katika Tuzo za NBAA za mwaka 2024 kwa kundi la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), chini ya kipengele cha Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha kwa taasisi zinazotumia Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa Sekta ya Umma (IPSAS).

CPA Damasco Peter, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MDH, pamoja na wafanyakazi wengine, walipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Wahasibu uliofanyika Bunju, Dar es Salaam.

Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb.)

Ambaye aliwapongeza washindi na kusisitiza kuwa kutambuliwa huko kuwe ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa manufaa ya taasisi zao na taifa kwa ujumla.

