Mdhamini wa Amber Rutty Aingia Mitini, Arudishwa Rumande – Video

VIDEO Vixen wa Bongo, Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’ na ‘bwana’ke’, Said Mtopari, wamerudishwa Gereza la Segerea baada ya kukosa mdhamini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2018.
Kesi hiyo iliyokuwa ikiendelea leo Jumatatu, mahakamani hapo, ilikuja kwa ajili ya kutajwa ambapo watuhumiwa (Amber Rutty na mpenzi wake) walitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini bondi ya Tsh. Milioni 15 kila mmoja, lakini alijitokeza mdhamini mmoja pekee huku mmoja akikosekana.
Mshtakiwa Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa. Kesi imeahirisha hadi Desemba 10, 2018.
Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na makosa ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, 
kuchapisha video/picha za ngono na kusababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp.

BREAKING: Kesi ya Amber Rutty Wadhamini Wamtosa Mahakamani

Loading...

Toa comment