Mdogo wa Kanumba Hoi Kitandani

MDOGO wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco yupo hoi kitandani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la mwili kufa ganzi.

 

Seth amepatwa na tatizo hilo ambapo mwili wake kuanzia sehemu ya kiunoni hadi miguuni, viungo vyote havifanyi kazi.

 

“Nina kama wiki ya pili sasa tangu niletwe hapa Muhimbili, mwili haufanyi kazi kuanzia kiunoni hadi miguuni. Kabla ya hapo hali hii ilinijia ghafla tu. Nimefanyiwa vipimo na madaktari wameniambia natakiwa kufanyiwa upasuaji hivyo nasubiria,” alisema Seth.


Loading...

Toa comment